Swali: Kuna mtu anayewasomea watu Ruqyah kupitia TV na mtu huyo anatoka nje ya nchi hii. Anakhusisha nyakati mbali mbali kisomo maalum cha kijicho, kingine cha jini, kingine cha hasadi na kadhalika. Ni yapi maoni yako juu ya hilo?

Jibu: Huku ni kucheza na Ruqyah. Ruqyah inasomewa moja kwa moja mgonjwa kwa kuwepo kwake mbele. Hasomewi mtu ambaye yuko mbali. Huku ni kucheza na Ruqyah na kuitoa mahala pake. Kwa masikitiko makubwa mnajua kuwa leo kumekithiri uchezaji na walaji wanaokula pesa za watu ambao wanawasomea watu kupitia simu na TV. Yote haya ni kucheza na Ruqyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020