Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua picha kwa video camera? Je, hilo linaingia katika kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah awalaani watengeneza picha”?

Jibu: Ndio, inaingia. Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jumla:

“Allaah awalaani watengeneza picha.”

“Kila mtengeneza picha ni Motoni.”

Hakukuvuliwa kitu. Picha haijuzu, sawa ikiwa kwa njia ya video camera wala kifaa kingine. Lakini hata hivyo, baadhi ya wanachuoni wa leo wamefutu kuwa ni sawa kupiga picha wakati wa dharurah. Kwa mfano leseni ya kuendesha, kitambulisho n.k. Hizi ni picha za dharurah ambazo mtu hawezi kujitosheleza nazo kutokana na maslahi yake. Hizi ni picha za dharurah. Zimeruhusiwa kwa dharurah. Yanaruhusiwa kwa dharurah yasiyoruhusiwa kwa mengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020