Uhakikishaji wa kunyonya kati ya wanandugu unafanywa na Qaadhiy

Swali: Kuna mtu ameoa na amezaa na mke wake watoto. Kisha baadaye ikaionekana kuwa mke wake alinyonyeshwa na mama yake. Ni ipi hukumu kwa hili?

Jibu: Huyu aenda kwa Qaadhiy. Huyu aenda kwa Qaadhiy na amlete mnyonyaji na amuulize. Unyonyaji ukisihi kwa masharti yake watenganishwe. Watoto ni wa kwake kwa kuwa wanaingia katika watoto walio na utata. Wanamfuata [baba yao]. Qaadhiy ndiye ana haki ya kuwatenganisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020