Mwanafunzi mwenye haki ya kutoa darsa

Swali: Ni zipi sifa za mwanafunzi ambaye ana haki ya kutoa duruus, khutbah, mihadhara na nasaha kwa ´Awwaam na vijana?

Jibu: Awe anamcha Allaah na asizungumze juu ya Allaah pasina elimu. Asizungumze isipokuwa kwa kile anachokijua. Akiulizwa kuhusi kitu asichokijua aseme kuwa Allaah ndiye Anajua zaidi. Asiwe na ujasiri kwa Allaah wala kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Azungumze kwa elimu iliyojengwa juu ya Qur-aan, Sunnah na maneno ya wanachuoni.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2697
  • Imechapishwa: 01/05/2015