Swali: Unamnasihi kitu gani mtu ambaye masomo yanamzuia kuoa? Vipi kijana atakusanya kati ya kuoa na masomo?

Jibu: Ikiwa anaweza kusoma kwa muda wa mwaka, miwili, mitatu mpaka mine bila ya kuoa ili aweze kufikia elimu yenye manufaa ni bora. Ikiwa hawezi hilo na akaoa, achague na kuoa mwanamke mwema ambaye atamsaidia kusoma. Nimemwambia ayape kipaumbele masomo kwa muda kwa sababu wanawake wengi wa leo hawawasaidii waume zao na kusoma. Wana mahitajio mengi. Wanataka hiki na kile. Anataka awaige wanawake wengine na kueleza yale waliyo nayo wengine. Isipokuwa tu wale waliorehemewa na Allaah na ni wachache mno.

Vijana wengi wanapinda wakati wanapooa. Wanapinda na kutafuta elimu. Kwa kuwa yuko na mke wa dunia na wa maslahi. Hamu yake kubwa ni mambo ya kidunia. Anachojali yeye ni mambo ya kidunia; kula, kunywa, kuvaa, kutoka na kupoteza wakati. Hasaidii kutafuta elimu. Ndio maana anatakiwa kutafuta elimu.

Wakati ameshatafuta elimu asioe mwanamke ni mwanamke. Ajaribu kuoa mwanamke mwenye Dini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Oa mwanamke mwenye Dini, mikono yako ifunikwe na mchanga.”

Awe nimwanamke mwema na msafi.

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako: “Ikiwa mnataka uhai wa dunia na mapambo yake; basi njooni nikupeni kiliwazo (kitoka nyumba) na nikuacheni huru (talaka) mwachano mzuri.” (33:28)

Bi maana awataliki:

وَإِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا

“Na ikiwa mnamtaka Allaah na Mtume Wake na nyumba ya Aakhirah, basi hakika Allaah Amewaahidi Muhsinaat (wanawake watendao wema) miongoni mwenu ujira adhimu.” (33:29)

Katika zama za Salaf ndoa ilikuwa ni katika mambo bora yanayosaidia kusoma. Baada ya hapo ndoa ikaja kuwa ni katika mambo makubwa yanayomzuia mtu kusoma. Yote haya huanza kidogo kidogo. Kisha yanakuwa. Mahitajio yanazidi kuwa mengi. Pale ambapo mtoto tu anakuwa mgonjwa anakimbizwa hospitali. Imekuwa hakuna tena kumtegemea Allaah. Imekuwa hakuna tena subira. Kwa kitu kidogo. Hawataki hata nguo iliolowa impate mtoto. Pale tu anaposhikwa na homa kidogo anakimbizwa hospitali. Kitambaa kidogo tu kilicholowa kinatosheleza. Hadiyth inasema:

“Homa ni katika moto wa Jahannam. Hivyo basi ipozeni kwa maji.”

Hata kitu kidogo kama hichi kinatunzwa. Moja kwa moja ataenda hospitali.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2697
  • Imechapishwa: 01/05/2015