Swali: Unawanasihi nini wale wenye mapicha majumbani?

Jibu: Ninawanasihi kuziondosha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataa kuingia nyumba yake mwenyewe na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) kwa sababu ya picha. Hakuingia mpaka wakati ´Aaishah alipoiondosha. Allaah Amesema:

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرً

“Kwa hakika mna kigezo kizuri kwa Mtume wa Allaah kwa kwa mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho na akamtaja Allaah kwa wingi.” (33:21)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Malaika hawaingii nyumba ilio na picha na mbwa.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni watengeneza picha.”

Amewalaani watengeneza picha na kusema:

“Kila mtengeneza picha yuko Motoni.”

Isipokuwa tu picha wakati wa dharurah kama pasipoti, leseni ya kuendesha na kitambulisho. Allaah Anasema:

فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

”Lakini aliyefikwa na dharura pasi na kutamani wala kupindukia mpaka, basi si dhambi juu yake. Hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (02:173)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2697
  • Imechapishwa: 01/05/2015