Swali: Kuna mtu ana mfanya kazi kwenye kilimo. Mfanya kazi huu anaswali lakini hafungi Ramadhaan bila ya udhuru wa Kishari´ah pamoja na kuwa kazi sio ngumu. Je, amwache au abadilishe mwingine?

Jibu: Abadilishe mwingine. Allaah Anasema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Shirikianeni katika wema na kumcha Allaah, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)