1. Faida ya pili: Umefaidika pia kuwa na khofu kubwa.

MAELEZO

Ukiitambua Tawhiyd sahihi na ukatambua shirki mbaya, basi hayo yatakufidisha kuwa na khofu juu ya yale waliyotumbukia watu wengi katika kwenda kinyume na msingi huu na kutumbukia katika shirki pasi na wewe kujua. Usijiamini nafsi yako na wala usidanganyike na matendo yako au uelewa wako. Lakini unachotakiwa ni kusema ´hapana hila wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah` na umuombe Allaah uthabiti. Hakika Ibraahiym, ambaye ni kipenzi wa Allaah wa hali ya juu, ambaye alipewa elimu na yakini ambayo haikupewa yeyote yule isipokuwa Mtume anasema:

وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ

“Uniepushe mimi na wanangu kuabudu masanamu. Mola wangu! Hakika hao wamepoteza wengi sana katika watu.” (14:35)

Ibraahiym haikujiaminisha nafsi yake fitina pamoja na elimu na yakini yake ilihali yeye ndiye ambaye aliyavunja masanamu kwa mkono wake na akawekwa kwenye moto kwa sababu hiyo. Pamoja na haya anachelea juu ya nafsi yake fitina. Kwa hiyo usidanganyike kwa matendo yako na ukaiaminisha nafsi yako kutokamana na fitina. Badala yake unatakiwa daima kuchukua tahadhari kutokamana na fitina ukaja kuteleza na ukaghurika na kitu ambacho ikawa ndio sababu ya kuangamia kwako na upotevu wako.

Baadhi ya waliodanganyika hii leo wanasema kuwa watu wamepita kile kiwango cha ujinga na uchumi na wamekuwa ni wenye ufahamu na kwa ajili hiyo ndio maana haingii akilini eti wakarudi katika [´ibaadah za] mizimu au wanasema mfano wa maneno kama haya ya kipuuzi. Ni kana kwamba hawafahamu ´ibaadah za makaburi zilizoenea katika miji mingi ya Kiislamu na hawakuangalia ule ujinga walionao watu wengi juu ya Tawhiyd.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 52
  • Imechapishwa: 28/11/2016