Swali: Kwa mfano mtu anapomtembelea mgonjwa amwombee du´aa, amtemee cheche za mate au aseme:

أسأل الله العلي العظيم رب العرش العظيم أن يشفيك

“Namuomba Allaah Mtukufu, Mola wa ´Arshi tukufu, akuponye.”

kisha ataje jina la mtu huyo?

Jibu: Amuombee du´aa. Du´aa ni jambo zuri. Akimtembelea ndugu yake amwombee du´aa. Kuna unyonge katika Hadiyth hii. Lakini kuna matarajio kwake kujibiwa:

أسأل الله العلي العظيم رب العرش العظيم أن يشفيك

“Namuomba Allaah Mtukufu, Mola wa ´Arshi tukufu, akuponye.”

Aombe mara saba.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21589/هل-يوجد-دعاء-مشروع-عند-عيادة-المريض
  • Imechapishwa: 18/08/2022