115 – Zitazame nyota kwa uchache iwezekanavyo, isipokuwa kwa yale yatayokusaidia kujua nyakati za swalah. Jiepushe na yote yasiyokuwa hayo, kwani hakika yanaita katika uzandiki.
116 – Tahadhari na kutazama katika elimu ya falsafa na kukaa pamoja na watu wa falsafa.
117 – Lazimiana na masimulizi (الآثار) na watu wa masimulizi (أهل الآثار). Waulize wao, keti pamoja nao na chuma kutoka kwao.
118 – Tambua ya kuwa Allaah hajapatapo kuabudiwa kama kuwa na khofu juu Yake. Njia za khofu, huzuni, huruma na haya zinatokamana na Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).
119 – Tahadhari kukaa pamoja na wanaoita katika shauku na mapenzi, wenye kukaa faragha na wanawake na mfumo wa madhehebu, hakika watu wote hawa wamo upotofuni.
120 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewaita viumbe wote katika kumuabudu Yeye na amewaneemesha Uislamu wale anaowataka kutokana na fadhilah Zake.
- Muhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 110-111
- Imechapishwa: 23/12/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
15. Hivyo ndio hutokea upotofu wa kidini
81 - Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona na Mjuzi. Mikono Yake miwili imekunjuliwa. Allaah alijua kuwa viumbe Wake watamuasi kabla ya kuwaumba. Ujuzi Wake ni kutendeka juu yao. Ujuzi Wake juu yao haikumzuia kuwaongoza katika Uislamu na kuwatunuku kwa sababu ya ukarimu na fadhilah Zake -…
In "Sharh-us-Sunnah - al-Barbahaariy"
20. Wapumbavu pekee ndio huzua
102- Tambua ya kwamba hakukuja Bid´ah yoyote isipokuwa kutoka kwa watu duni, wapumbavu na wafuasi wa kila mwenye kupiga ukelele. Wanaenda na kila upepo. Ambaye hali yake ni kama hii, basi hana dini yoyote. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema: فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ "Basi…
In "Sharh-us-Sunnah - al-Barbahaariy"
28. Ukimuona mtu anakaa na wazushi
145 - Ukimuona mtu anakaa na mtu katika wazushi, basi mtahadharishe na mzindue. Akiendelea kukaa nao baada ya kujua, jitenge mbali naye; kwani hakika huyo naye ni mzushi. 146 - Ukisikia mtu mwenye kuyasikia masimulizi na hali ya kuwa hayataki, badala yake anataka Qur-aan, usitie shaka ya kwamba ni mtu…
In "Sharh-us-Sunnah - al-Barbahaariy"