23. Unaotakiwa na usiotakiwa kutangamana nao

115 – Zitazame nyota kwa uchache iwezekanavyo, isipokuwa kwa yale yatayokusaidia kujua nyakati za swalah. Jiepushe na yote yasiyokuwa hayo, kwani hakika yanaita katika uzandiki.

116 – Tahadhari na kutazama katika elimu ya falsafa na kukaa pamoja na watu wa falsafa.

117 – Lazimiana na masimulizi (الآثار) na watu wa masimulizi (أهل الآثار). Waulize wao, keti pamoja nao na chuma kutoka kwao.

118 –  Tambua ya kuwa Allaah hajapatapo kuabudiwa kama kuwa na khofu juu Yake. Njia za khofu, huzuni, huruma na haya zinatokamana na Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

119 – Tahadhari kukaa pamoja na wanaoita katika shauku na mapenzi, wenye kukaa faragha na wanawake na mfumo wa madhehebu, hakika watu wote hawa wamo upotofuni.

120 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewaita viumbe wote katika kumuabudu Yeye na amewaneemesha Uislamu wale anaowataka kutokana na fadhilah Zake.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 23/12/2024