Je, nia ni sharti ya kukusanya baina ya swalah mbili?

Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kwamba ni sharti kuwa na nia ya kukusanya swalah kabla ya kuanza swalah?

Jibu: Haya ndio yaliyotangaa, lakini sahihi ni kwamba nia si lazima. Kwa mfano mtu ameswali Maghrib kisha punde ikaanza kunyesha mvua kubwa. Katika hali hiyo inajuzu kwake kukusanya na ´Ishaa. Vilevile ikiwa mtu alianza kuswali Maghrib akiwa mzima, kisha punde akapatwa na ugonjwa, inafaa kwake kukusanya kwa mujibu wa maoni sahihi ambayo yamechaguliwa na Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah na kikosi cha wanazuoni wengine. Jengine ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa anawaambia kuwa anakusanya swalah. Alikuwa akiswali Maghrib na hakuwa akiwatangazia kwamba ataunganisha. Vivyo hivyo anaposwali Dhuhr. Kwa hivyo ikafahamisha ya kwamba si sharti.  Kwani kama nia ingekuwa ni sharti, basi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angewaambia kabla ya kwamba watakusanya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24756/هل-النية-شرط-للجمع-بين-الصلاتين
  • Imechapishwa: 23/12/2024