Ni lini wakati wa mwisho wa ´Ishaa?

Swali: Ni wakati gani wa mwisho wa swalah ya ´Ishaa?

Jibu: Ni nusu ya usiku, kama ilivyoelezwa katika hadithi ya ´Abdullaah bin ´Amr. Huu ndio wakati wake wa mwisho. Ikiwa mtu ataswali baada ya theluthi ya usiku, kwa namna ya kwamba watu wamekubaliana kufanya hivyo kwa pamoja katika msikiti kwa sababu ni jambo linalowafaa, hapana vibaya. Kadri inavyocheleweshwa ndio bora zaidi…. Hata hivyo ikiwa hakuna makubaliano kati ya waumini wa misikiti inayojulikana, basi ni bora kutochelewesha. Hii ni kwa sababu watu wana mahitaji yao. Ni vizuri kuchelewesha ´Ishaa kidogo tu na kisha watu waswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24774/متى-اخر-وقت-العشاء
  • Imechapishwa: 23/12/2024