102- Tambua ya kwamba hakukuja Bid´ah yoyote isipokuwa kutoka kwa watu duni, wapumbavu na wafuasi wa kila mwenye kupiga ukelele. Wanaenda na kila upepo. Ambaye hali yake ni kama hii, basi hana dini yoyote. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:
فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ
“Basi hawakukhitilafiana isipokuwa baada ya kuwajia elimu kwa uhusuda baina yao.”[1]
وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ
“Hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa baada ya kuwajia hoja za wazi – kwa uhusuda baina yao.”[2]
Hawa ni wale wanazuoni waovu na watu wa matamanio na wa Bid´ah.
103 – Tambua ya kwamba siku zote kutaendelea kuwepo kikundi kutoka katika Ahl-ul-Haqq was-Sunnah. Allaah atawaongoza na awaongoze wengine kupitia wao. Kupitia wao Ataihuisha Sunnah. Hao ndio wale Allaah (Ta´ala) aliowaelezea pamoja uchache wao wakati wa kutofautiana. Amesema:

“Basi hawakukhitilafiana isipokuwa baada ya kuwajia elimu – kwa uhusuda baina yao.”
Kisha Akawabagua na kusema:
فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗوَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
“Ndipo Allaah akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana kwa idhini Yake – na Allaah humwongoza amtakaye katika njia iliyonyooka.”[4]
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kikundi katika ummah wangu kitaendelea siku zote kuwa ni chenye kushinda juu ya haki. Hakitodhurika na wale wenye kuwakoseshwa nusura mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ilihali bado ni wenye kushinda.”[5]
104 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba elimu sio mtu kuwa na masimulizi na vitabu vingi; isipokuwa mwanachuoni ni yule mwenye kufuata elimu na Sunnah, ijapo atakuwa na elimu na vitabu vichache. Yule mwenye kwenda kinyume na Kitabu na Sunnah, basi huyo ni mtu wa Bid´ah. Haijalishi kitu hata kama atakuwa na masimulizi na vitabu vingi.
105 – Tambua – Allaah akurehemu – yule mwenye kusema kuhusu dini ya Allaah kwa maoni, kipimo na tafsiri yake bila ya kuwa na dalili kutoka katika Sunnah na Mkusanyiko, atakuwa amesema juu ya Allaah asichokijua. Na yule mwenye kusema juu ya Allaah asichokijua, huyo ni katika wenye kujikalifisha.
[1] 45:17a
[2] 02:213
[4] 02:213
[5] Muslim (1924)
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 102-104
- Imechapishwa: 23/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 102-104
Imechapishwa: 23/12/2024
https://firqatunnajia.com/20-wapumbavu-pekee-ndio-huzua/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)