106 – Haki ni ile ambayo imekuja kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Sunnah ni njia ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mkusanyiko ni ile waliyokusanyikaemo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ukhalifah wa Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan.

107 – Ambaye atatosheka na Sunnah zake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mfumo wa Maswahabah zake na Mkusanyiko, basi atawashinda Ahl-ul-Bid´ah wote, utastarehe mwili wake na dini yake itasalimika – Allaah akitaka. Haya ni kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu utafarikiana katika mapote sabini na tatu.”

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa ametubainishia kundi lenye kuokoka katika wao na akasema:

“Ni wale wataokuwemo katika yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Hii ndio ponyo na ubainifu, jambo la wazi na mnara unaotoa nuru. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jihadharini na kupetuka mipaka na kuingia kwa ndani zaidi na jilazimisheni na dini yenu ya kale.”[1]

108 – Tambua kuwa dini ya kale ni ile iliyosheheni tangu alipokufa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka alipouawa ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh). Kuuawa kwake ndio ilikuwa chanzo cha mfarakano na tofauti. Ummah wa Kiislamu ukapigana vita na kufarikiana na hivyo ukafuata matamanio. Ukaanza kumili katika mambo ya kilimwengu. Hakuna yeyoye aliye na ruhusa ya kuzua kitu katika mambo ambayo hawakuwemo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kadhalika inahusiana na mtu mwenye kulingania katika kitu kilichozushwa na Ahl-ul-Bid´ah kabla yake. Mtu huyo ni kama yule aliyekizusha. Mwenye kudai hivyo au akazungumza kwa jambno hilo, basi ameirudisha Sunnah na kwenda kinyume na haki na Mkusanyiko.  Ameruhusu Bid´ah na atakuwa ni muovu zaidi katika ummah huu kuliko Ibliys.

109 – Mwenye kuzijua zile Sunnah ambazo watu wa Bid´ah wameziacha na kuzikhalifu na yeye akawa ameshikamana nazo, huyo ni mtu wa Sunnah na mtu wa Mkusanyiko. Ana haki ya kufuatwa, kusaidiwa na kuhifadhiwa na mtu huyo ni katika watu waliopendekezwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bayhaqiy katika ”al-Madkhal” (388).

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 105-107
  • Imechapishwa: 23/12/2024