145 – Ukimuona mtu anakaa na mtu katika wazushi, basi mtahadharishe na mzindue. Akiendelea kukaa nao baada ya kujua, jitenge mbali naye; kwani hakika huyo naye ni mzushi.

146 – Ukisikia mtu mwenye kuyasikia masimulizi na hali ya kuwa hayataki, badala yake anataka Qur-aan, usitie shaka ya kwamba ni mtu aliye na uzandiki. Simama kutoka kwake na achana naye.

147 – Tambua kuwa matamanio yote ni maovu. Yote yanaita kwenye upanga. Mabaya zaidi kati yao ni Raafidhwah, Mu´tazilah pamoja na Jahmiyyah, hakika wanachotaka ni kuwaongoza watu katika ukanushaji na uzandiki.

148 – Tambua ya kwamba mwenye kumshambulia yeyote katika Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), anachotaka ni kumshambulia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amemuudhi ndani ya kaburi lake.

149 – Ukidhihirikiwa na kitu katika Bid´ah kutoka kwa mtu, basi tahadhari naye. Kwani hakika yale aliyokuficha ni mengi kuliko yale aliyokudhihirisha.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 121-123
  • Imechapishwa: 30/12/2024