150 – Ukimuona mtu katika Ahl-us-Sunnah ambaye njia na mwenendo wake ni mbaya na ni mtenda dhambi, muovu, mtenda maasi na mpotevu na wakati huohuo yuko katika Sunnah, tangamana naye na keti naye, hakika maasi yake hayatokudhuru. Ukimuona mtu ni mwenye kujitahidi na kujipinda katika ´ibaadah, mwenye kuipa kisogo dunia na mwenye bidii kweli katika ´ibaadah na wakati huohuo akawa ni mzushi, usiikae naye, usiyasikilize maneno yake na wala usitembee naye kwenye njia, kwani mimi nachelea usije kuridhia njia yake na hatimaye ukawa ni mwenye kuangamia pamoja naye[1]. Yuunus bin ´Ubayd alimuona mwanawe akitoka kwa bwana mmoja katika wazushi na akasema:
“Ee mwanangu, umetoka wapi?” Akasema: “Kutoka kwa fulani.” Akamwambia: “Ee mwangu! Napendelea zaidi kukuona unatoka kwenye nyumba ya huntha kuliko kukuona unatoka kwenye nyumba ya fulani na fulani. Ee mwanangu! Napendelea zaidi ukutane na Allaah hali ya kuwa ni mzinifu, mtenda dhambi, mwizi na mfanya khiyana kuliko ukutane Naye na maoni ya fulani na fulani.”[1]
Huoni kuwa Yuunus bin ´Ubayd alitambua kuwa huntha hawezi kumfanya mwanawe akapotea kutokana na dini yake, ilihali mtu wa Bid´ah anaweza kumpotosha mpaka akakufuru.
151 – Tahadhari na khaswa khaswa na watu wa zama zako na tazama ni nani unakaa naye, ni nani unamsikiza na kusuhubiana naye, kwani ni kana kwamba viumbe wako katika kuritadi – isipokuwa wale waliokingwa na Allaah.
152 – Chunga ukimsikia mtu anamtaja Ibn Abiy Du-aad, Bishr al-Maariysiy, Thumaamah, Abu Hudhayl, Hishaam al-Fuutwiy au yeyote katika marafiki na wafuasi wao. Katika hali hiyo tahadhari naye, kwani hakika ni mtu wa Bid´ah. Watu hawa walikuwa katika kuritadi. Achana na mtu huyu ambaye anawasema vizuri na yule aliyemtaja katika wao.
[1] Abu Nu´aym (03/20-1), al-Khatwiyb al-Baghdaadiy katika “Taariykh Baghdaad” (12/172-173) na wengineo.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 123-126
- Imechapishwa: 30/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 123-126
Imechapishwa: 30/12/2024
https://firqatunnajia.com/29-usifanye-urafiki-na-mzushi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)