30. Hakuna kusikia neno hata moja kutoka kwa mzushi

153 – Kuwatia wengine katika mtihani ni jambo la Bid´ah. Ama kuhusu leo wanapewa mtihani kwa Sunnah, kutokana na maneno yake:

“Hakika elimu hii ni dini. Hivyo basi, kuwa mwangalifu ni kutoka kwa nani mnaichukua dini yenu.”[1]

Pia:

“Msiikubali Hadiyth isipokuwa kutoka kwa yule mnayekubali ushuhuda wake.”[2]

Kwa hivyo unatakiwa kuangalia. Ikiwa mtu ni mtu wa Sunnah, mjuzi na ni mkweli, andika kutoka kwake. Vinginevyo achana naye.

154 – Ukitaka kuwa na msimamo juu ya haki na kuwafuata waliokuwa kabla yako walioko katika njia ya Ahl-us-Sunnah, tahadhari na falsafa na wenye kujishughulisha na falsafa, mijalada, ubishi, kipimo na magomvi katika dini. Hakika kuwasikiliza kwako – hata kama hutokubali kitu kutoka kwao – kunapenyeza shaka ndani ya moyo. Kunatosheleza mtu akayakubali na akaangamia. Hakupatapo kamwe kuwepo uzandiki, Bid´ah, matamanio wala upotevu, isipokuwa ni kwa ajili ya falsafa, mijadala, ubishi na kipimo. Yote haya ndio mlango wa Bid´ah, mashaka na uzandiki.

155 – Jikumbushe nafsi yako juu ya Allaah. Jilazimishe na masimulizi, watu wake na yafuate. Hakika hapana vyenginevyo dini ina maana ya kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake na Maswahabah zake. Waliokuwa kabla yetu hawakutuacha katika utatizi. Wafuate, ustarehe na usiyavuke masimulizi na watu wake.

156 – Simama katika yenye kutatiza na wala usilinganishe kitu.

157 – Usitafute hila ambazo kwazo ukafikiria kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah. Umeamrishwa kuwanyamazia na wala usiwape fursa juu ya nafsi yako. Hujui ya kwamba Muhammad bin Siyriyn – pamoja na fadhilah zake – hakumjibu mtu kutoka katika Ahl-ul-Bid´ah katika suala moja tu? Hakukubali kusikia Aayah japo moja kutoka katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall). Alipoulizwa juu ya hilo akasema:

“Ninachelea asije kuipotosha na hivyo kukaingia kitu ndani ya moyo wangu.”[3]

[1] Ibn ´Adiy katika “al-Kaamil” (01/155), as-Sahmiy katika “Taariyk Jarjaan”, uk. 473 na Ibn-ul-Jawziy katika “al-Waahiyaat” (01/131). Shaykh Khaalid ar-Raddaadiy (Hafidhwahu Allaah) amesema:

“Mnyororo ni dhaifu sana kwa sababu ya Khaalid bin Du´luj ambaye ni dhaifu mno, kama ilivyotajwa katika “al-Miyzaan” (01/352-353).” Lakini hata hivyo maneno haya yamesihi kutoka kwa Imaam Muhammad bin Siyriyn (Rahimahu Allaah) na yanapatikana kwa Muslim (01/31), “al-Kaamiyl” (01/155) ya Ibn ´Adiys, Abu Nu´aym (02/278) na wengineo. (Taaliki ya Sharh-us-Sunnah” (153))

[2] Imezuliwa kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf al-Jaamiy´” (6193).

[3] ad-Daarimiy (01/91), Ibn Wadhdhwaah katika “al-Bid´ah”, uk. 53 na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 126-128
  • Imechapishwa: 30/12/2024