Kumtii khaliyfah na watawala wengine ni jambo la lazima katika mambo yasiyokuwa kumuasi Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kusikiliza na kutii kwa muislamu ni jambo la lazima katika anayoyapenda na kuyachukia muda wa kuwa hajaamrishwa maasi. Akiamrishwa maasi, basi hakuna kusikiliza wala kutii.”[2]
Kuna maafikiano juu yake.
Ni mamoja kiongozi huyo ni mwema, kwa msemo mwingine anatekeleza maamrisho ya Allaah hali ya kuyafanya na kuyaacha, au ni muovu ambaye anatenda madhambi makubwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Zindukeni! Yule ambaye atatawalishiwa mtawala na akaona anafanya kitu katika maasi, basi achukie yale anayoyaona katika kumuasi Allaah na asiondoe mkono kutoka katika utiifu.”[3]
Ameipokea Muslim.
Hajj na jihaad zinakuwa endelevu na zenye kutekelezwa pamoja na viongozi. Ni sawa kuswali nyuma yao swalah ya ijumaa. Ni mamoja ni wema au waovu. Kwa sababu kupingana nao katika hayo kunapelekea kufarikisha umoja na waislamu na kuwaasi.
[1] 04:59
[2] al-Bukhaariy (7144) na Muslim (1839, 38).
[3] Muslim (1855, 66).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 157
- Imechapishwa: 17/12/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Haijuzu kumtii yeyote katika maasi
Swali 10: Tunamuomba baba mlezi muheshimiwa neno kuhusu bay´ah juu ya watawala Saudi Arabia? Jibu: Ni wajibu kwa waislamu wote katika nchi hii ya Saudi Arabia kusikiliza na kuwatii watawala kwa wema, kama zilivyofahamisha juu ya hilo Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa na kuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).…
In "Daar-ul-Islaam na Daar-ul-Kufr"
Yeye ndiye mpotevu
Swali: Unasemaje juu ya yule mwenye kusifu wale wenye kuita katika kumtii mtawala ya kwamba ni "watiifu walopetuka mipaka"? Jibu: Waache waseme wanavyotaka. Kusikiliza na kutii ni katika mambo yaliyoamrisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ…
In "al-Fawzaan kuhusu sifa na alama za Ahl-ul-Bid´ah"
Serikali inakataza biashara ya halali
Swali: Je, inafaa kwa yeyote kukataza kitu kilichoruhusiwa? Ibn ´Uthaymiyn: Kivipi? Swali: Serikali ikamkataza mtu kufungua biashara ambayo imeruhusiwa. Je, atii jambo hilo? Jibu: Ni lazima kwa mtu kumsikiliza na kumtii mtawala muda wa kuwa sio katika maasi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Ni lazima kwa muumini kusikiliza…
In "Ibn ´Uthaymiyn msimamo kwa watawala"