Swali: Unasemaje juu ya yule mwenye kusifu wale wenye kuita katika kumtii mtawala ya kwamba ni “watiifu walopetuka mipaka”?

Jibu: Waache waseme wanavyotaka. Kusikiliza na kutii ni katika mambo yaliyoamrisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.” (04:59)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninakuusieni kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mtumwa.”

Haya yameamrishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule kupuuzia yale aliyoamrisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio mkoseaji na mpotevu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2020