Hadiyth iliyotajwa na mtunzi wa kitabu:

“Mambo matatu ni katika msingi wa imani: Kukomeka na aliyetamka “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” hatumkufurishi kwa dhambi wala kumtoa katika Uislamu kwa kitendo na Jihaad itaendelea kuwepo tangu aliponituma Allaah (´Azza wa Jall) mpaka pale Ummah wangu wa mwisho utapompiga vita ad-Dajjaal – hayaangushwi na unyanyasaji wa mwenye kunyanyasa wala uadilifu wa mwenye kufanya uadilifu. Aidha kuamini Qadar.”

ni dhaifu. Hayo yameashiriwa na as-Suyuutwiy katika “al-Jaamiy´-us-Swaghiyr” na kuna mpokezi ambaye al-Mizziy amesema kuwa hatambuliki. at-Tirmidhiy amesema katika “Mukhtaswar Abiy Daawuud: “Hatambuliki.”

Kumfanyia uasi kiongozi ni jambo la haramu. ´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikula kiapo cha usikivu kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) juu ya kusikiza na kutii, katika uchangamfu wetu na yale tunayoyachukia, katika kipindi chepesi na kigumu, pindi mtu anapopendelewa juu yetu na kwamba tusivutane na watawala mpaka pale mtakapoona ukafiri wa wazi ambao tuna dalili kwao kutoka kwa Allaah.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtatawaliwa na viongozi ambao mtayakubali mambo na mengine mtayakaaa. Yule ambaye atayakataa basi ameepukana [na dhambi] na yule ambaye atachukia basi amesalimika. Lakini [dhambi ni kwa] ambaye ataridhia na kufuata. Wakasema: “Je, tusiwapige vita?” Akasema: “Hapana, muda wa kuwa wanaswali.”[2]

Ameipokea Muslim.

Bi maana atakayepinga na kuchukia kwa moyo wake.

Miongoni mwa faida za Hadiyth mbili ni kwamba kuacha swalah ni ukafiri wa wazi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakujuzisha kufanya uasi kwa viongozi isipokuwa kunapopatikana ukafiri wa wazi. Amefanya kikwazo cha kuwapiga vita ni kule kuswali. Kwa hivyo inafahamisha kuiacha kunahalalisha kuwapiga vita. Kuwapiga vita hakuhalalishwi isipokuwa kutokana na ukafiri wa wazi, kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Ubaadah.

[1] al-Bukhaariy (7055, 7056) na Muslim (1709, 42).

[2] Muslim (1854, 63, 64).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 157-158
  • Imechapishwa: 17/12/2022