Zawadi inayotolewa katika kumfanyia mtu uombezi

Swali: Imekuja katika Hadiyth ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliona Swafiyyah amechukulia vibaya ambapo Swafiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akamwambia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Je, unaonaje umridhishe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nikupe siku yangu… ?”

Kuna jambo lenye kutatiza katika Hadiyth: je, zawadi inakubaliwa katika uombezi?

Jibu: Hapana, isipokuwa akiliruhusu hilo mume. Mume alikiruhusu hilo haina neno.

Swali: ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikubali siku ya Swafiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa)?

Jibu: Ni siku ya Sawdah. Sawdah alipotaka kuachwa akamwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa anamgawia siku yake ´Aaishah ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akalikubali hilo. Kwa hivyo ni sawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikubali kutoka kwa mke wake.

Swali: Haizingatiwi kuwa ni katika kukubali zawadi katika uombezi?

Jibu: Hapana, haina neno. Kwa sababu huku ni kudondosha haki yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23096/ما-حكم-الهدية-التي-تعطى-في-الشفاعة
  • Imechapishwa: 01/11/2023