Swali: Baadhi wanajengea hoja kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko hai ndani ya kaburi lake kwa kitendo cha Malaika kumfikishia swalah na salamu ndani ya kaburi lake.

Jibu: Roho yake iko Peponi. Anafikishiwa salamu. Roho yake iko Peponi katika ngazi ya juu kabisa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanamfikishia salamu. Roho yake iko hai. Roho hazifi. Kinachokufa ni kiwiliwili. Kufa kwa roho ni kule kutoka kwake kwenye viwiliwili. Huku ndio kufa kwake. Ni kama ilivyotajwa katika Hadiyth Swahiyh:

“Roho za waumini ni ndege zinazoruka Peponi na roho za mashahidi ziko ndani ya matumbo ya kijani zinaruka Peponi popote zinapotaka. Halafu zinarudi kwenye kwenye lile taa.”

Kwa hivyo miili ndio inayoteketea isipokuwa kifupa kilicho kwenye uti wa mgongo wa mtu (عجب الذنب). Roho zinabaki. Roho za waumini ziko Peponi na roho za makafiri ziko Motoni. Tunamuomba Allaah usalama. Hakuna kizuizi chochote katika baadhi ya nyakati Allaah akitaka kuirudisha roho kwenye kiwiliwili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23097/هل-النبي-عليه-الصلاة-والسلام-حي-في-قبره
  • Imechapishwa: 01/11/2023