4 – Shaddaad bin Aws (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jitofautisheni na mayahudi. Kwani hakika wao hawaswali na soksi zao za ngozi wala viatu vyao.”[1]

[1] Abu Daawuud (652) na Ibn Hibbaan (3186). Nimeitaja katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuuud” (659) na huko tumewataja wale maimamu walioisahihisha. Nimetaja pia tafsiri yake katika ”ath-Thamar al-Mustatwaab” na katika ”Swifatu Swalaat-in-Nabiy”. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kujitofautisha na mayahudi katika kila kitu. Ni dalili inayojulisha kuwa kule kujitofautisha kwenyewe ni lengo linalotakikana katika Shari´ah.  Katika hali hii kutaja kuswali ndani ya viatu na soksi za ngozi sio kukhusisha kilichoenea au kufungamanisha kilichoachiwa, bali ni mfano tu wa kigezo chenye kuenea. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hukumu iko namna hii ingawa uvuaji wa viatu kwa mayahudi ni jambo lina msingi kwa Muusa (´alayhis-Salaam) pale alipoambiwa:

إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى

”Hakika Mimi ni Mola wako, hivyo vua viatu vyako, kwani hakika wewe uko katika bonde takatifu la Twuwaa.” (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 29)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 172
  • Imechapishwa: 01/11/2023