Zawadi au mwaliko wa anayefanya kazi ya haramu

Swali: Je, mtu akubali zawadi ya ambaye kazi yake ni ya haramu au mchango wake wa kujenga misikiti au matendo mengine ya kheri?

Jibu: Uchaji zaidi ni mtu kutokupokea. Vinginevyo kama tulivyotangulia kusema dhambi zinampata yule mfanyaji. Tumesema kuwa dhambi zinampata yule mtendaji kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitaamiliana na mayahudi ilihali wanakula ribaa na huenda wakati mwingine wanamwalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo anaitikia mwaliko wao ilihali ni walaji ribaa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 10/09/2023