Pale ambapo umelazimishwa kulipa bima

Swali: Ni ipi hukumu ya bima juu ya nafsi na pesa na ndani yake kunakuwa na mbinu za kuchukua pesa kutoka kwa makafiri?

Jibu: Bima hii haijuzu. Maadui wa Uislamu wanatumia pesa kwa ajili  ya manufaa yao katika benki za ribaa na wanafaidika pesa nyingi. Isipokuwa ikiwa kama umelazimishwa. Tunalipa ushuru, forodha kwa magari na vingine ijapo sisi tunaitakidi kuwa ni haramu. Ikiwa umelazimishwa basi jihadhari kuhadaika na makafiri. Usiwahadae. Ikiwa wanawapiga vita katika uwanja basi ni juu yako kufanya kile unachoweza. Vita ni hadaa. Lakini kitendo cha wewe kuwahadaa katika pesa kinafanya wakawa na dhana mbaya juu ya Uislamu na waislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 59
  • Imechapishwa: 10/09/2023