Zakaah juu ya pesa iliokuwa imepotea baada ya miaka mingi

Swali: Kuna pesa zangu nilizozificha maeneo fulani kisha nikasahau pesa hizo kwa miaka mingi. Baadaye nikazipata kwa bahati tu. Nitazitolea kiasi gani pesa hizi kwa sababu sijui ni miaka mingapi imezipitia?

Jibu: Hazitolewi zakaah juu ya ile miaka iliyopita. Ni pesa iliyopotea. Zakaah itakuwa wajibu kuanzia pale ulipozipata. Hapo ndipo utazitolea zakaah juu ya mwaka mmoja. Nao ni ile mwaka ambao umezipata ndani yake peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 02/04/2023