Sifa za Allaah ni katika Aayah zenye kutatiza?

Swali: Msemo huu ni sahihi:

”Aayah zote kuhusu sifa za Allaah (´Azza wa Jall) ni katika Aayah zisizokuwa wazi na hivyo sisi… ”

Jibu: Tunamuomba Allaah usalama. Sifa za Allaah sio katika Aayah zenye kutatiza. Aayah zisizokuwa wazi ni zile ambazo hazijulikani maana yake. Sifa za Allaah zinajulikana maana yake. Mu´tazilah, Ashaa´irah na wapotofu wengine ndio ambao wanaona kuwa sifa za Allaah ni katika Aayah zisizokuwa wazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 02/04/2023