Mwanamke anasafiri peke yake kwenda kwa mume wake

Swali: Ni ipi hukumu mwanmke kusafiri bila ya kuwa na Mahram pamoja na kuzingatia kwamba atafika katika uwanja wa ndege na kupokelewa katika uwanja wa ndege wa pili kwa lengo la kwenda kwa mume wake huko?

Jibu: Hebu nikuulize kwanza kama una dhamana ya yeye kufika katika uwanja wa ndege wa pili? Au kuna uwezekano ndege ikabadilisha mwelekeo na kuruka katika mji mwingine na kudema katika uwanja mwingine wa ndege kutokana na sababu miongoni mwa sababu? Katika hali hiyo ni nani atakayempokea? Ni maneno gani haya? Ni nani ambaye anaweza kudhamini kuwa ndege daima hudema katika mahali ambapo ilikusudia? Hutokea mambo na hivyo ikadema mahali mwingine. Ni nani ambaye atampokea mwanamke huyu atakapofika katika mji wa kigeni ambapo hakuna yeyote wa kumpokea?

Ama tunapokuja upande wa dalili, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwa njia ya kuenea. Huku inaenea kila zama na kila mahali na kila chombo cha usafiri. Amesema kwa njia ya kuenea:

”Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Ni nani ambaye anaweza kufanya maalum na kusema kwamba anasafiri kwa ndege na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakujua kuwa kutakuja ndege? Allaah ametakasika kutokana na mapungufu! Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni yenye kuenea kila zama na kila mahali. Shari´ah ya Kiislamu ni yenye kuenea mpaka kusimame Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 02/04/2023