Wote isipokuwa tu shahidi aliyekufa uwanja wa vita

Swali: Je, mtu aliyezama ndani ya maji na aliyeangukiwa na jengo wanaswaliwa?

Jibu: Ndio, mashahidi wote wanaswaliwa isipokuwa tu yule shahidi aliyekufa uwanja wa vita. Ni kama alivooshwa na kuswaliwa ´Umar, ´Uthmaan na wengineo.

Swali: Wanaoshwa pia?

Jibu: Wanaoshwa, wanavikwa sanda na kuswaliwa. Isipokuwa tu yule shahidi aliyekufa na kuuliwa katika uwanja wa vita.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22883/هل-يصلى-على-الغريق-والمهدوم
  • Imechapishwa: 09/09/2023