Kufa na deni ni sababu ya kuadhibiwa kaburini?

Swali: Anaadhibiwa ndani ya kaburi aliyekufa na mkopo?

Jibu: Ikiwa alizembea na kupuuza ni dhambi na hivyo yuko khatarini. Lakini ikiwa ana uzito na si kwamba amekusudia kufanya kwa kutaka kwake, hayuko khatarini:

وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ 

”Na ikiwa [mdaiwa] ni mwenye hali ngumu, basi [anayedai] angoje mpaka afarijike.”[1]

[1] 02:280

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22886/هل-الدين-من-اسباب-عذاب-القبر
  • Imechapishwa: 09/09/2023