Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali swalah ya Witr msikitini kwa mkusanyiko?

Jibu: Haijuzu kudumu kuswali Witr kwa mkusanyiko. Haijalishi kitu msikiitini au kwenginepo. Isipokuwa katika Ramadhaan baada ya swalah ya Tarawiyh. Mbali na wakati huo kila mmoja anatakiwa kuswali Witr peke yake. Bora Witr iswaliwe mwishoni mwa usiku. Isipokuwa asiyekuwa na uhakika wa kuamka mwishoni mwa usiku basi anaweza kuswali Witr mwanzoni mwake.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaDetails.aspx?View=Page&PageID=12218&CultStr=ar&PageNo=1&NodeID=1&BookID=3
  • Imechapishwa: 17/04/2022