Kulipa Witr ambayo hakuiswali kwa sababu ya hedhi

Swali: Kuna mwanamke ameswali ´Ishaa na hakuswali Witr kwa kukusudia kuamka usiku sehemu iliyobakia ya usiku. Wakati ilipokuwa theluthi ya mwisho ya usiku akapata hedhi. Je, alipe Witr yake aliyoacha pamoja na kuzingatia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo maishani kuacha Sunnah ya Fajr na Witr katika hali ya ukazi wala hali ya safari?

Jibu: Miongoni mwa mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba alikuwa inapompita Witr usiku kutokana na maradhi au kupitiwa na usingizi basi anailipa mchana kabla ya jua kupondoka hali ya shufwa. Kwa hivyo mtu akichelewesha kulipa Witr mpaka baada ya kipindi hicho basi haikusuniwa kwake kukidhi kile kilichompita.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaDetails.aspx?View=Page&PageID=12219&CultStr=ar&PageNo=1&NodeID=1&BookID=3
  • Imechapishwa: 17/04/2022