Swali: Katika hali ya kukusanya ´Ishaa na Maghrib kwa sababu ya mvua inafaa kwa mtu baada ya swalah ya ´Ishaa akaswali shufwa na witr msikitini baada ya kumalizika swalah ya mkusanyiko ya ´Ishaa au ni lazima kwake asubiri mpaka ufike wakati wa ´Ishaa kisha ndio aswali Sunnah, shufwa na witr? Ni lipi bora?

Jibu: Swalah ya ´Ishaa ikikusanywa na Maghrib katika wakati wa magharibi kutokana na udhuru unaokubalika ki-Shari´ah basi itafaa kuswali Witr baada yake. Kuichelewesha mpaka mwishoni mwa usiku ndio bora mtu akiweza kufanya hivo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alifta.gov.sa/Ar/IftaContents/Pages/FatawaDetails.aspx?View=Page&PageID=12220&CultStr=ar&PageNo=1&NodeID=1&BookID=3
  • Imechapishwa: 17/04/2022