Watoto chini ya miaka saba msikitini

Swali: Kuwaleta msikitini wavulana chini ya miaka saba.

Jibu: Bora ni kuwaacha watoto wa miaka saba muda wa kuwa kuna wepesi wa kufanya hivo ili wasiwashawishi watu. Lakini haudhuru ikiwa wataletwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mimi wakati mwingine nasikia kilio cha mtoto na nikafupisha swalah.”

Lakini hakuwakataza. Wakati mwingine anaweza kuhitajia kuja. Anaweza kulazimika kuja naye kwa sababu hakuna yeyote wa kumwangalia. Pengine mama yake hayuko nyumbani, ameachika, ameshakufa au mayatima wadogo ambao hawana wa kuwaangalia. Lakini akishafikisha maiaka saba basi anatakiwa kuswali na wengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22511/حكم-حضور-الصغار-دون-السابعة-للمسجد
  • Imechapishwa: 17/06/2023