Dhuhaa haina kikomo cha wingi wa Rak´ah

Swali: Je, mtu aswali Sunnah ya Dhuhaa kila siku?

Jibu: Ni Sunnah yenye kudumu na kila siku. Uchache wa Rak´ah zake ni mbili. Hakuna kikomo cha wingi wa Rak´ah zake; Rak´ah nne, nane, kumi au mia. Hapana neno. Lakini uchache wake ni Rak´ah mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22541/هل-يشرع-المداومة-على-صلاة-الضحى
  • Imechapishwa: 17/06/2023