Swali: Ninapoanza Swalah hupatwa na wasiwasi kwa aina ya kwamba nimevunja nia au ninaswali kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Hivyo hukata Swalah na kuanza upya. Unaninasihi nini?

Jibu: Ninakunasihi uachane na wasiwasi huu. Unatokama na Shaytwaan. Zipuuzie fikira hizo zenye kusema kuwa hukusema “Allaahu Akbar”, huna Wudhuu na umekatika… Achana na wasiwasi huu na utupilie mbali kabisa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331123.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015