Wasiwasi au ni kujiepusha na vitu vyenye utata?

Swali: Kuacha kula nyama zinazotoka nje kwa kuchelea kuwa hazikuchinjwa kwa njia inayokubalika kiislamu ni katika wasiwasi au ni katika kujiepusha na vitu vyenye utata?

Jibu: Ni katika kujiepusha na vitu vyenye utata. Zina utata kwa sababu hawachinji kwa njia inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Wanachinja kwa pamoja au wanachinja kwa kumweka mnyama ndani ya maji ya moto kisha baadaye wanamkata shingo yake baada ya kwamba ameshakufa. Yote haya yanatajwa juu yao. Kwa hiyo zina utata. Kule kuziacha kwako ni katika kujiepusha na vitu vyenye utata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 19/05/2023