Amesafiri miezi miwili kwenda hajj na mke wake mmoja

Swali: Nilienda hajj na mke wangu mmoja na nikabaki naye huko kwa muda wa miezi miwili. Je, inanilazimu kubaki na mke wangu wa pili kwa kiasi cha miezi miwili?

Jibu: Hapana. Umepewa udhuru kutokana na safari yako. Hivyo unatakiwa kuanza kugawa zamu kati ya wake zako kuanzia mwanzo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 19/05/2023