Wasichana wadogo wasivishwe suruwali

Swali: Una nasaha gani kuwapa wale ambao wanachukulia wepesi kuwavisha suruwali wasichana wadogo na mavazi yanayoonyesha uchi kwa hoja eti bado eti hawajabaleghe. Wanachukulia nasaha ni katika kuwa na msimamo mkali…

Jibu: Hapana, haijuzu kufanya hivo. Wasichana wadogo wasilelewi juu ya mavazi yenye kuonyesha uchi na kutokuwa na haya. Wasileleki juu ya hayo. Waleleke juu ya heshima, mavazi na kujisitiri. Akileleka juu ya hayo atakuwa nayo. Haijuzu kuchukulia wepesi mambo haya na kusema bado ni mdogo. Mdogo anatakiwa na kuhitaji kulelewa. Anatakiwa kuzoezwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (03)
  • Imechapishwa: 25/02/2024