Swali: Unasemaje mwanamke kumnasihi mwanaume kwa njia ya kuamrisha mema na kukemea maovu?

Jibu: Ndio, mwanamke ananasihi:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[1]

Mwanamke naye anatakiwa kuamrisha mema na kukemea maovu. Yeye ni kama mwanamme.

[1] 09:71

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (04)
  • Imechapishwa: 25/02/2024