Wanataka kumfungia mama lakini hawajui anadaiwa siku ngapi

Swali: Mama yangu alipofariki alikuwa anadaiwa siku kadhaa za mwezi wa Ramadhaan na hatujui siku hizi ni ngapi kutokana na wingi wa kula kwake kwa sababu ya ugonjwa wa pumu. Alikuwa ananuia kulipa lakini hata hivyo akafa. Je, yepi yanayotulazimu?

Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwenu kumfungia. Imesuniwa kwenu kumfungia kwa kiasi cha dhana. Mjitahidi na mfunge vile inavyopelekea dhana yenu kubwa ya siku alizokula za Ramadhaan na mtakuwa wenye kulipwa thawabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayekufa na anadaiwa swawm, basi atafungiwa na walii wake.”

Bi maana ndugu zake.

Bora kwenu ni kumfungia yale ambayo yatakuwepesikia wewe na dada zako wengine au mmoja wenu anaweza kumfungia vile inavyopelekea dhana yake. Mkidhani kuwa ni siku kumi basi mfunge siku kumi. Mkidhani kuwa ni siku kumi na tano basi mfunge siku kumi na tano. Vivyo hivyo vile inavyopelekea dhana yenu na itatosha kufanya hivo. Vilevile inatosha mkimtolea chakula kumpa masikini kwa kila siku moja aliyokula. Lakini bora ni nyinyi kufunga kwa niaba yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9549/كيفية-الصيام-عن-مات-ولا-يعلم-عدد-الايام-التي-افطرها
  • Imechapishwa: 27/03/2023