Swali: Du´aa ya mfungaji hairudishwi nyuma. Hili ni nyakati zote au ni wakati wa kukata swawm?

Jibu: Mchana wote ni wakati wa kukata swawm. Katika hali ya funga yake na wakati wa kukata kwake swawm.

Swali: Kwa mfano wakati  anapoadhini muadhini?

Jibu: Wakati wa kukata swawm, adhuhuri, alasiri na nyakati nyenginezo zote za mfungaji. Mfungaji ana du´aa yenye kujibiwa wakati wa kufunga kwake na pia wakati wa kukata kwake swawm. Hapo ni pale atakaposalimisha na vikwazo vingine kama kula haramu na maasi mengine. Kwa sababu kukubaliwa kuna vikwazo vyake pia katika madhambi, maasi, kula ribaa na mambo mengine ya haramu. Tunamuomba Allaah salama.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22774/متى-وقت-دعوة-الصاىم-التي-لا-ترد
  • Imechapishwa: 27/03/2023