Inafaa kwa mwanamme na mwanamke kuchelewesha deni mpaka katika Sha´baan

Swali: Je, inafaa kulipa siku nilizokula za Ramadhaan katika kumi la mwisho la Sha´baan au kabla yake kwa nisba ya mwanamke?

Jibu: Hapana vibaya kwa nisba ya mwanamke na mwanamme wote wawili. Inafaa kuchelewesha ulipaji mpaka katika Sha´baan. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anahaa) alikuwa akichelewesha mpaka Sha´baan. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“… hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Hakutenga wakati maalum na wala hakusema kuwa ni lazima kuharakisha. Ikafahamisha kuwa jambo ni lenye wasaa. Inasihi akilipa siku za Ramadhaan katika Shawwaal, Dhul-Qa´adah, Dhul-Hijjaah, Muharram, Swafar na miezi mingine.

[1] 02:184

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10551/حكم-تاخير-قضاء-رمضان-الى-شعبان
  • Imechapishwa: 27/03/2023