Ameugua na kuingiliwa na Ramadhaan nyingine

Swali: Mimi ni mwanamke ambaye ni mgonjwa na nilikula baadhi ya siku za Ramadhaan iliyotangulia na sikuweza kulipa kwa sababu ya ugonjwa wangu. Ni ipi kafara ya hilo? Kadhalika siweza kufunga Ramadhaan ya mwaka huu. Ni ipi kafara ya hilo pia?

Jibu: Mgonjwa ambaye inakuwa vigumu kwake kufunga inasuniwa kwake kula. Atalipa zile siku anazodaiwa pale Allaah atapomponya. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

”Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi [atimize] idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Hakuna vibaya kwako kula ndani ya mwezi huu maadamu bado ni mgonjwa. Kula ni ruhusa ya Allaah kwa mgonjwa na msafiri. Allaah anapenda zitendewe kazi ruhusa Zake kama anavochukia kuasiwa. Hulazimiki kutoa kafara. Lakini ni lazima kwako kulipa pindi Allaah atapokuponya. Allaah akuponye na kila baya na atusamehe sote makosa yetu.

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/353)
  • Imechapishwa: 27/03/2023