Swali: Baada ya kuolewa kwa miaka thelathini kuna mtu mwaminifu aliwaambia ya kwamba mume na mke ni ndugu wa kunyonya. Na kwa sasa wana watoto wa kike na wa kiume na mume amekwishakufa (Allaah Amrehemu). Je, watoto wana Ahkaam za Kishari´ah na yeye na mume wake wana madhambi?

Jibu: Warejee mahakamani kwa hilo. Warejee mahakamani kwa hilo. Ahudhurie vilevile yule mwenye kudai kuwa walinyonya pamoja mahakamani ili muweze kufutiwa juu ya hilo. Kwa kuwa hili ni jambo muhimu na ni jambo kubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12796
  • Imechapishwa: 19/11/2014