Kulala baada ya ´Aswr na baina ya Maghrib na ´Ishaa

Swali: Baba yangu analala kuanzia wakati wa Swalah ya ´Aswr mpaka Maghrib, kisha kuanzia wakati wa Maghrib mpaka ´Ishaa bila ya Swalah kumpita. Je, nina madhambi lau nitamnasihi kwa kuwa mimi napenda awe macho katika wakati huu kwani hilo ni bora kwake?

Jibu: Ama kulala baada ya ´Aswr haina neno. Hakukuthibiti kinachotolea dalili kukataza. Ama kulala baina ya Maghrib na ´Ishaa imechukizwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anachukia kulala kabla yake na kuongea baada yake (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Imechukizwa kulala baada ya Maghrib kwa wanaume na wanawake. Ni vizuri kumuamsha na kumnasihi. Ama asli jambo hili ni sahali Alhamdulillaah.

  • Mhusika: Imaaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=155
  • Imechapishwa: 19/11/2014