Swali: Lau muislamu atapeana mikono na myahudi au mnaswara wakati yuko na wudhuu´. Ana nini juu yake?

Jibu: Haifai kwake kupeana mikono na kafiri. Asimpe mkono. Akitoa salamu aseme: “wa ´alaykum.” Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ahl-ul-Kitaab wakiwatolea salamu, semeni: “wa ´alaykum”.”

Asianze kumsalimia yeye na wala asimpe mkono. Lakini ikiwa yeye ataanza kukupa mkono na kukusalimia, wudhuu´ wake hauvunjiki. Wudhuu´ wake ni sahihi. Kumgusa kafiri hakutengui wudhuu´.

  • Mhusika: Imaaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=155
  • Imechapishwa: 19/11/2014