Wakazi wengi wa Peponi ni mafukara

Swali: Hadiyth inasema:

“Nimetazama Peponi na nimeona wakazi wake wengi ni mafukara.”

Ibn-ul-Qayyim ametaja kuwa fitina ya mali ni kubwa zaidi kuliko fitina ya shida na ufukara.

Jibu:

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ

”Hakika si venginevyo mali zenu na watoto wenu ni jaribio.”[1]

Swali: Je, hapo tunapata faida kuwa watiifu na wema mara nyingi wanakuwa ni mafukara ijapo wanapatikana matajiri wachache?

Jibu: Hivi ndio mara nyingi. Ni kama ilivyokuwa kwa Maswahabah.

[1] 64:15

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22203/هل-فتنة-المال-اعظم-من-فتنة-الفقر
  • Imechapishwa: 05/11/2022