Nimesikia kalima ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Barraak ambapo anamuwaidhi Yuusuf al-Qaradhwaawiy. Hakika amefanya vibaya sana. Ni kipi kinachomfanya kujiingiza kumwandikia mfalme – Allaah amuwafikishe – na anamshukuru kwa kadhaa na kadhaa na anamtaka afanye kadhaa na kadhaa. Kwa nini asiwakataze watu kufanya shirki kubwa wakati anapokaa katika msikiti wa al-Husayn? Huwezi kuwapata al-Ikhwaan al-Muslimuun wakikataza shirki kubwa. Hamu yao kubwa ni utawala wa kisiasa iwe ya kiislamu.

Bwana huyu anamwandikia mfalme na kumtaka wanawake waendeshe gari. Allaah amjaze kheri Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Barraak kwa aliyoyaandika na amwongoze Yuusuf al-Qaradhwaawiy.

Yuusuf al-Qaradhwaawiy alisafiri kwenda Iraan na miji mingine na kuwafanya waislamu wawe na umoja. Ni vipi waislamu watakuwa na umoja juu ya njia moja wakati ambapo wako ambao wanamuwekea nadhiri Husayn, wanamwomba al-Husayn, wanamtaka msaada na wanaona kuwa kwenda katika kaburi lake ni bora kuliko kwenda kuhiji Makkah?

Swali: Msimamo wa Yuusuf al-Qaradhwaawiy juu ya vyombo vya mawasiliano na khaswa maandamamo, baadhi wanahoji kwa kuuliza ni vipi mwanachuoni atamkosa mwanachuoni mwingine hadharani na kwa nini wasinasihiane siri? Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Wakati mimi hapo nyuma nilipozungumza Haram na nikasema kuwa kumfanyia uasi mtawala kwa kufanya maandamano ni kueneza ufisadi ardhini na kwamba maandamano ya kwanza katika Uislamu ilikuwa ni sababu ya kuuliwa kwa ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh), alisema kuwa al-Luhaydaan amekosea katika hili na kwamba ni lazima kufanya maandamano kwa ajili ya kutokomeza unyanyasaji.

Lakini yule anayejua mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun na akasoma maelekezo yao inapokuja katika haki na kulazimiana na maamrisho, ataona kuwa hawako juu ya ´Aqiydah sahihi na iliyotakasika.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=NnDo-gn8a6g&feature=related
  • Imechapishwa: 05/11/2022